Walemavu Walalamikia Kutengwa Kilifi

Mwanaharakati wa kutetea haki za wenye ulemavu mjini Malindi kaunti ya Kilifi Willy Mwangi amelelamikia hatua ya wao kutengewa kiasi kidogo cha fedha katika bajeti ya mwaka wakifedha wa 2020/2021.

Akizumgumza na meza yetu ya habari Mwangi amesema kuwa watu wanaoishi na ulemavu wamekuwa wakitoa mapendekezo yao katika bajeti ya miaka ya hapo awali na huenda kupungua kwa mgao wao kumechangiwa na hatua ya wao kutoweza kufika katika maeneo ya kutoa maoni yao kama njia moja ya kuwasilisha mapendekezo yao.

Also Read
Wanachama Wa Bodi Ya Inuka Funds Wasailiwa Tana River
Also Read
Kero La Ndovu Taita Taveta

Mwangi ametaja hatua ya wale wanaohudhuria mikutano hiyo kuwa na uwoga wa kutoa mapendekezo yao kwa kile alichokisema kuwa wanakosa ujasiri wa kusisimama na kutoa maoni yao jambo ambalo huenda likawa limechangiwa na unyanyapaa kutoka kwa jamii.

Also Read
Vijana Wahimizwa Kutunza Na Kuenzi Utamaduni Kilifi

Hata hivyo amesema kuwa zipo baadhi ya fedha ambazo zimekuwa zikitengwa ili kuwajengea kituo cha kuwaimarisha lakini bado swala hilo halijawai fanikiwa licha ya wao kuchukua jukumu la kutaka kujua sababu kuu ya wao kutojengewa vituo hivyo.

  

Latest posts

Vijana Wametakiwa Kutosubiri Kupewa Pesa Na Wanasiasa Ili Wajiandikishe Kama Wapiga Kura

Clavery Khonde

Wakaazi Taita Taveta Wahimizwa Kupokea Chanjo Dhidi Ya Korona

Clavery Khonde

Ken Chonga Akanusha Madai Ya Ubadhirifu Wa Fedha Za Basari

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi