Kamishna wa kaunti a Kilifi Kutswa Olaka anawata walimu ambao wanadhulumiwa kwa kupigwa na wanafunzi na wazazi kuripoti visa hivyo kwa idara ya usalama kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Olaka visa vya walimu kupigwa haviripotiwi kwa idara ya usalama ili uchunguzi ufanywe ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Akizungumza mjini Kilifi Olaka amesema naibu mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Kachororoni eneo bunge la Ganze ambaye anadaiwa kupigwa na wazazi hajaandikisha taarifa kwa polisi.
Vile vile kamishna huyo amesema wameweka mikakati ya kuhusisha washikadau mbali mbali ili kuhakikisha visa kama hivyo havitokei mashuleni.
Aidha amewataka wazazi kufuata mkondo wa sheria na kutatua matatizo baina yao na walimu kwa njia inayostahili bila mivutano.