Wanahabari wahimizwa kuzingatia maadili ya taalum yao kaunti ya Kwale

Wanahabari wa kaunti ya Kwale wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wanapopeperusha habari na jumbe zilizosawa ili kuhakikisha kuwa hazipotoshi ummma.

Akiongea katika kikao na wanahabari, gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amesema kumekuwa na ongezeko la baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii kusambaza uvumi unaolenga kupotosha wananchi.

Also Read
Kingi awataka maseneta kuwajibika bungeni kwa manufaa ya mwananchi mashinani

Mvurya amesema ipo haja ya wanahabari kutafuta usawa na kutathmini habari wanazoandika kabla ya kufahamisha umma.

Also Read
Wakaazi Walioathirika Na Ujenzi Wa Bwawa La Mwache Wadai Fidia

Hata hivyo Mvurya amewapongeza wanahabari kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamisisha umma dhidi ya janga la korona.

Also Read
Serikali Ya Kaunti Ya Kwale Yahimizwa Kukamilisha Ujenzi Wa Barabara

Haya yanajiri baada ya baadhi ya wananchi kaunti ya Kwale kusambaza habari za uvumi hali walioitaja kuleta wasiwasi.

  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi