Wanaharakati wa Maswala Ya Mihadarati Wasema Wanafunzi Wanaochoma Shule Wengi Hutumia Mihadarati

Idadi kubwa ya wanafunzi wanaotajwa kuhusika na visa vya uchomaji wa shule ni wale wanaojihusisha na utumizi wa dawa za kulevya katika taasisi hizo.

Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati katika kaunti ya kilifi Famau Mohammed Famau, ambaye amesema kuwa idadai kubwa ya vijana aina hiyo huwashawishi weingine kuwaunga mkono katika kutekeleza utovu huo wa nidhamu shuleni.

Also Read
Mamamke Trio Mio amfrusha Meneja wiki mbili  baada Trio kuenda shuleni

Katika taarifa yake kwa wanahabari eneo hili, Famau amesema kuwa ipo haja ya serikali kuchukua jukumu la kutekeleza uchunguzi dhidhi ya wanafunzi hao na hata kuwachukulia hatua za kisheria.

Also Read
Pombe ya Kienyeji Yenye Mchanganyiko wa Ndizi Yauwa Watu 11 Rwanda

Famau amedai kuwa shughuli za ulanguzi wa dawa za kulevya, zimekuwa zikiendelezwa katika taasisi za elimu jambo ambalo limepelekea baadhi ya wanafunzi , kupata bidhaa hizo kwa urahisi.

Also Read
Gavana Kingi Asutwa

Aidha ameitaka serikali kuanzisha mpango wa kutoa ushauri nasaha kwa baadhi ya wanafunzi , watakao patikana kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya shuleni.

  

Latest posts

Kaunti ya Kilifi yaanza uboreshaji wa huduma za afya

Joshua Chome

Bunge lajadili hotuba ya rais huku mseto wa hisia ukiibuka kutoka kwa pande mbili

Joshua Chome

Rais wa Uganda Yoweri Museveni awaomba msamaha Wakenya kwa jumbe kutoka kwa generali Mohoozi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi