Wanaoshiriki Ushirikina Kanisani Wakemewa

Mchungaji  wa kanisa Jesus Victory Joel Masika kaunti ya Mombasa amekemea tabia ya  waumini wa dini ya Kikristo katika ukanda  wa Pwani kuenda kwa waganga ili kutafuta suluhu la matatizo yao.

Also Read
Usalama Kuimarishwa Wakati Wa Uchaguzi Asema Matiang'i

Akizungumza na meza yetu ya habari, mchungaji Joel amekitaja kitendo hicho kuwa kinyume na imani ya kikristo.

Masika amesema kwamba ni hali ya kusikitisha kuwaona  waumini  ambao wanapaswa kuiweka imani yao kwa Mungu na kumuomba bila kuchoka wanachukua maamuzi ya kutafuta msaada kwa waganga.

Also Read
Shahbal Amsuta Abdulswamad Shariff Nassir

Aidha mchungaji Joel ameelezea athari zinazoshuhudiwa baada ya Wakristo kutafuta suluhu la matatizo yao kwa waganga huku akisema tabia hizo zinaenda kinyume na neno la Mungu kwenye kitabu kitakatifu.

  

Latest posts

Wafanyibiashara Katika Soko La Malindi Walalamikia Uchafu na Uvundo.

Sylvester Chibero

Wakenya Wametakiwa Kuwa Waangalifu Wakati Wanapoabiri Magari Msimu Huu Washerehe.

Sylvester Chibero

Tutashamiri Kwenye Mashindano Ya Mwaka Huu Ya Tong-IL Moo Do Asema Master Mwakio

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi