Viongozi wa kidini mjini Malindi kaunti ya Kilifi wamekashifu swala la madhabahu kutumika na wanasiasa kupiga siasa wanapotembelea makanisa.Wakiongozwa na mchungaji Edward Fondo wa kanisa la Neema Baptist hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi amesema kuwa Madhabahu ni mahali patakatifu na kamwe hapapaswi kutumika katika maswala ya kisiasa.
Akizungumza na meza yetu ya habari mchungaji Fondo ameeleza kuwa hatua ya kuruhusu wanasiasa kutumia madhabahu hunajisi sehemu hiyo ambayo lengo lake kuu ni kueneza injili ya Mungu na wala sio siasa.
Aidha mchungaji huyo amewaonya wachungaji wengine dhidi ya kujiunga na siasa kwa kile alichokisema kuwa ni njia mojawapo inayo dhihirisha kutowajibikia kazi ya Mungu kwani mtu huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati moja.