Wakaazi wa eneo la pwani wamehimizwa kukumbatia viongozi wanaogombea kupitia chama cha Pamoja African Alliance PAA.
Wakiongea katika kongamano la wajumbe wa chama hicho mjini Kilifi viongozi hao wamewahimiza wakaazi hao kuhakikisha kuwa wanaleta mageuzi ya viongozi na kusambaratisha utawala wa chama cha ODM
Mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Rabai Kenga Mupe ameahidi kuwa chama hicho kitatoa viongozi wengi katika ngazi ya kitaifa na ndani ya eneo la pwani.
Ni kauli iliyoungwa mkono na mgombea wa ubunge eneo la Ganze Kenneth Charo Tungule akisema kuwa yeye anaimani kubwa na kumbwaga mbunge wa sasa Teddy Mwambire kwenye eneo hilo la Ganze.