Kwa akali watu saba wameuawa huku wengine zaidi ya 140 wakijeruhiwa katika makabiliano baina ya waandamanaji na maafisa usalama nchini Sudan.
Maandamano hayo yalianza baada ya jeshi la Sudan kuvunja serikali ya mpito iliyokuwa inajumuisha raia na wanajeshi na wakati huo huo kuwakamata viongozi wa kisiasa akiwemo Waziri Mkuu, sanjari na kutangaza hali ya hatari nchi nzima.
Kufuatia uamuzi huo wa jeshi, waandamanaji wenye hasira walimiminika kwenye barabara za mji mkuu, Khartoum na kuwasha matairi barabarani huku milio ya risasi ikiendelea kusikika katika jiji hilo.
Jenerali Abdel Fattah Burhan, ambaye alikuwa akiongoza baraza la pamoja na viongozi wa kiraia, ametoa tangaza hilo na kusema mapinduzi ya sasa ya kijeshi yamesbabaishwa na malumbano ya kisiasa.