Wazazi Walio Na Watoto Ambao Wako Na Matatizo Ya Kimaumbile Wahimizwa Wajitokeze

Afisa wa mipango kuhusu rasilimali katika shirika la kuwashughulikia watu wenye mahitaji maalaum katika taasisi ya APDK ilioko eneo la Port Reitz Jemimah Kutata amewataka wazazi kutowaficha watoto wanaozaliwa na matatizo mbali mbali ya kimaumbile.

Also Read
ANC Yatoa Tiketi ya Moja Kwa Moja Kwa Muwaniaji wa Wadhfa Wa Uwakilishi Wadi Wa Bongwe

Kutata amesisitiza haja ya wazazi kuwachukulia watoto hao kama watoto wa kawaida na kujitokeza ili wapate usaidizi kutoka kwa mashirika kama vile APDK na mengineyo.

Kutata pia ameitaka jamii kuwa katika mstari wa mbele katika kuwakumbatia watoto hawa kama njia mojawapo ya kupunguza unyanyapaa ambao watoto hao hupitia.

Also Read
Wanafunzi Wapokea Dawa za Minyoo Mjini Mombasa

Kadhalika, amewarai wahisani kujitokeza ili kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.

Kutata aliyasema hayo katika hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtangazaji wa Pwani Fm Clemence Mkanyika Jilo ambaye alitoa msaada wa kiutu wa kuwasaidia watoto hao katika taasisi ya wa APDK ilioko eneo la Portreitz hapa Mombasa.

  

Latest posts

Kaunti ya Kilifi yaanza uboreshaji wa huduma za afya

Joshua Chome

Bunge lajadili hotuba ya rais huku mseto wa hisia ukiibuka kutoka kwa pande mbili

Joshua Chome

Rais wa Uganda Yoweri Museveni awaomba msamaha Wakenya kwa jumbe kutoka kwa generali Mohoozi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi