Wazee Wa Kaya Waunga Mkono Utunzi Wa Mazingira Magarini

Mshauri wa kundi la utamaduni eneo la Malindi kaunti ya Kilifi Edward Kazungu ambae ni mzee wa Kaya ameunga mkono kauli ya waziri wa mazingira nchini Keriako Tobiko ya kuwataka wenyeji kutunza miti katika eneo bunge la Magarini na Ukanda wa Pwani kwa jumla.
Akizungumza na wanahabari katika zoezi la upanzi wa miche ya Mikoko katika eneo la Sabaki Kazungu amesema kuwa ipo haja ya asasi zinazo husika na usalama wa mazingira kama vile NEMA.
Hata hivyo Kazungu ameongeza kuwa eneo la Sabaki litakuwa moja wapo ya vivutio vya watalii katika kaunti ya Kilifi baada ya serikali kutimiza ahadi yake ya kutenga eneo hilo kama moja wapo ya hifadhi za Serikali.
Aidha, kwa mujibu wa mmoja wa washika dau katika sekta ya Ukulima katika kaunti ya Kilifi Mwalimu Menza ameitaka serikali kuwapa kipaumbele wananchi katika maswala ya kutunza mazingira kwa kuwapa ajira katika sekta hiyo.

  

Latest posts

Nitaiboresha Idara Ya Usalama Kaunti Ya Mombasa Asema Abdullswamad Shariff Nassir

Clavery Khonde

Mpango Wa Wanawake Wazinduliwa Kwlae

Clavery Khonde

Waziri Magoha Aahidi Uimarishwaji Zaidi Wa Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi