Waziri wa Afya Mutahi Kagwe awahimiza walimu kutafakari kupata chanjo dhidi ya Covid-19

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amewahimiza walimu na wafanyakazi wengine shuleni kutafakari kupata chanjo dhidi ya Covid-19.

Kagwe alisema kuwa chanjo ziko na hivyo walimu na wafanyakazi wengine wanafaa kupata chanjo kwenye vituo vya afya ya umma bila malipo.

Also Read
Agizo La Waziri Kagwe La Kuwataka Wakenya Wachanjwe Dhidi Ya Korona Laungwa Mkono

Alisema kuwa ilhali watoto hawadhihirishi dalili za COVID-19, wanaweza kusambaza virusi hivyo kwa walimu wao.

Aliyasema haya kutokana na wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya maambukizi ya covid-19 shuleni lakini akawahakikishia wazazi kwamba hakuna sababu yoyote ya kuhofu.

Also Read
Chuo Cha Utalii Cha Ronald Ngala Kuanza Kuwapokea Wanafunzi Mwaka huu Asema Kibicho

Kagwe pia aliwahimiza wakenya wajiepushe na mikusanyiko ya kisiasa na kuzingatia kanuni za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo wanapohudhuria mazishi na harusi

Waziri aliyasema hayo wakati wa mkutano wa pamoja na wanahabari na mwenzake wa Tanzania Dr. Dorothy Gwajima,aliye humu nchini kwa mashauriano.

Also Read
Naibu rais Dkt William Ruto ajibu madai kuwa anamiliki kipande kikubwa cha ardhi Laikipia

Dr. Gwajima alisema kuwa ingawa Tanzania inatekeleza shughuli ya utoaji chanjo ili kukabiliana na COVID-19,bado wanatumia tiba za kiasili kujaliza tiba za kisasa.

  

Latest posts

EACC Itahakikisha Walioteuliwa Wanatia Saini Mkataba Wa Kujitolea

Ruth Masita

Haki Afrika Yaeleza Uchaguzi Wa Agosti 9 Haukuzingatia Haki

Ruth Masita

Mashirika Ya Kijamii Yaeleza Dosari Za Uchaguzi Mkuu Wa Tarehe 9 Agosti

Ruth Masita

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi