Waziri wa Utumishi wa Umma Atarajiwa Kutoa Taarifa Kuhusu Hali ya Ukame Nchini

Waziri wa utumishi wa umma, jinsia, maswala ya wakongwe na mipango maalum  Proffesor Margaret Kobia leo asubuhi anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu hali ya ukame humu nchini.

Waziri  Kobia anatarajiwa kuorodhesha mkakati maalum wa kugawa msaada wa chakula wa thamani ya shilingi bilioni 2.25 kwa shule katika kaunti 23 zinazoathiriwa na ukame. Hii ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasalia shuleni katika maeneo husika hasa wakati huu wa ukame. Shughuli hiyo itaandaliwa katika eneo la Nairobi Inland Container Depot huko Embakasi.

Also Read
Kilomita 8,000 mraba zachomeka kwenye jimbo la California
Also Read
Msongamano Wa Magari Ndani Ya Mji Wa Mombasa Waimarishwa

Serikali ilitabiri mwezi Septemba kuwa hali ya ukame itakuwa mbaya zaidi nchini katika mwezi wa Novemba na kufanya watu wapatao milioni  2.4 kuathirika na baa la njaa.

  

Latest posts

Mvurya Ataka Maafisa Wa Idara Na Mashirika Ya Serikali Kuhusu Maendeleo Zishirikishe Serikali Za Ugatuzi

Ruth Masita

Wanawake Wajasiriamali 450 Wanufaika Na Mafunzo Ya Kibiashara Mombasa

Ruth Masita

Mahakama yamwachilia mbunge wa Sirisia John Walukhe kwa dhamana ya shilingi milioni kumi

Joshua Chome

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi