William Maore Aibuka Mshindi Katika Shindano La Cocacola Almaarufu, ‘Under The Crown’

Vijana ambao ni wapenzi wa mchezo wa kandanda wametakiwa kuchukua fursa ya kushiriki kwenye mashindano ya bahati na sibu yanayofadhiliwa na kampuni ya Cocacola ili waweze kunufaika kimaisha.

Akizungumza na wanahabari katika afisi zao eneo la Kikambala kaunti ya Kilifi, afisa wa mauzo katika kampuni ya Cocacola eneo la Pwani Barry Otieno amesema kuwa ni kupitia mashindano hayo wanaweza kuwapa motisha vijana ambao ni wapenzi wa soka na wasiokuwa na ajira kujiendeleza kimaisha.

Kati ya washindi watano waliofanikiwa kupata zawadi kem kem sawa na tiketi ya kusafiri nchini Quatar kushuhudia kombe la dunia la FIFA 2022, William Maore ni mmoja wa hao washindi kutoka kaunti ya Mombasa.

Maore ni mfanyabiashara wa bodaboda katika barabara ya Bamburi mtambo na anaeleza furaha yake baada ya kupigiwa msimu na kampuni ya Cocacola.

Kombe la dunia la FIFA 2022 linatarajiwa kufanyika huko Quartar kwanzia tarehe 21 November hadi December tarehe 18.

  

Latest posts

Serikali ya kaunti ya Kilifi yatenga asilimia 15 ya bajeti kwa maendeleo

Joshua Chome

Kalonzo Aikosoa Serikali

Clavery Khonde

Rais Ruto Ateua Jopokazi Litakalo Tathmini Mtaala Wa CBC

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi