William Ruto Ajitenga na Siasa za Mlima Kenya

Kwa mara ya kwanza naibu raisi Dk. William Ruto amejitokeza wazi wazi na kujitenga na siasa za msitu wa Mau pamoja na kutoa msimamo wake hadharani kuhusiana na siasa za msitu huo akisema hakuhusika kivyovyote kupeleka watu ndani ya msitu wa Mau.

Also Read
Waziri Mkuu wa Libya Atangaza Azma Yake Ya Kuwa Rais

Aidha Ruto amesema wote waliotolewa kutoka kwa msitu huo hawataruhusiwa humo tena akisema hili linakwenda kumaliza siasa mbaya iliyokuwa ikizunguka sakata ya Mau.

Also Read
Chama cha Wiper kufungua ofisi Mombasa.

Akiongea mjini Narok naibu wa raisi ameahidi kwamba serikali itakwenda kujenga ua ili kuuzunguka msitu huo kama njia ya kuuhifadhi kutoka kwa wanyakuzi.

Akiwa kwenye ziara ya naibu wa raisi huko Narok mbunge maalum David Ole Sankok ameitetea kauli ya naibu wa raisi akisema walioupiga mapande msitu wa Mau wanajulika huku akiwataka wakaazi wa Narok kuunga mono sera ya botton-Up ujapo uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Wakaazi Wa Mombasa Wahakikishiwa Usalama Wao Katika Uchaguzi Mkuu Ujao
Naibu Rais William Ruto [kushoto] na David Ole Sankok [kulia]
  

Latest posts

Kiwango Cha Wateja Waliofurahia Huduma Za KRA Ndani Ya Miaka 3 Imeongezeka

Ruth Masita

HURIA Yalaumu Vyama Vya Kisiasa

Clavery Khonde

Wakaazi Kwale Waitaka Serikali Kushughulikia Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi