Chama cha Wiper Democratic Movement kimekanusha ripoti kwambaimemuidhinisha aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kuwania kiti cha ugavana Mombasa.
Katibu Mkuu Shakila Abdalla amesema kuwa chama hicho kilimpa tikiti ya moja kwa moja Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo kuwania kiti hicho.
Amesema Mbogo alipokea cheti hicho wakati wa kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama hicho huko Bomas of Kenya.
Hatua hiyo mpya inajiri baada ya fomu ya kuwasilisha kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), ambayo inaorodhesha wagombeaji vyama vya kisiasa vinavyonuia kuwasilisha kwa uteuzi wao kuvuja.
Orodha hiyo ilikuwa na jina la Sonko kama mmoja wa wanaowania chama.
Kulingana na orodha hiyo, gavana huyo wa zamani wa Nairobi anatarajiwa kumenyana na Mbogo kwenye mchujo wa Wiper.