Wito Watolewa kwa Wizara Ya Mazingira Kutambua Chemichemi za Maji Zilizofichika

Mkurugenzi wa chemichemi za maji kimataifa kanda ya Afrika Mashariki Julie Malonga ameitaka wizara ya mazingira nchini  kutambua kwa haraka na kuweka kwenye gazeti rasmi la serikali hifadhi zote za mikoko na chemi chemi za maji ambazo hazijatambuliwa na serikali.

Also Read
Uhaba wa Walimu Wasalia Kuwa Changamoto kwa CBC

Hatua hii inalenga  kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.

Kulingana na mkurugenzi huyo  ipo haja ya serikali kuteleza mpango huo kwa dharura ili kupunguza uharibifu wa mazingira katika sehemu husika.

Kauli hiyo imeungwa mkono na wadau mbali mbali wa kuhifadhi mazingira katika ukanda wa pwani.

Somo  Mohmaed Somo ni mvuvi kutoka kaunti ya Lamu.

Somo amesema mikoko huleta ongezeko la samaki.

Awali Waziri wa mazingira Keriako Tobiko alikuwa ametangaza kutambua na kuweka kwa jarida rasmi la serikali maeneo ya chemichemi za maji na misitu ambayo haijatambuliwa rasmi na serikali.

Waziri wa mazingira nchini Keriako Tobiko
  

Latest posts

Uteuzi Wa Karua Wapongezwa Na Wanawake

Clavery Khonde

Raila Amteua Martha Karua Kama Mgombea Mwenza Wake

Clavery Khonde

Wapwani Wahimizwa Kuunga Mkono Cha Cha PAA

Clavery Khonde

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Kubali Soma Zaidi