Idadi ya waliofariki katika jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini imefikia zaidi ya 300, kufuatia mafuriko yaliyosababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo.
Mamlaka za mitaa zinatoa wito wa hali ya maafa kutangazwa, baada ya baadhi ya maeneo kuona mvua ya miezi kadhaa kunyesha kwa siku moja.
Maafisa wameiita “moja ya dhoruba mbaya zaidi ya hali ya hewa katika historia ya nchi yetu”. Maporomoko ya udongo yamenasa watu chini ya majengo, huku mafuriko zaidi yakitarajiwa.
Juhudi za uokoaji zimeripotiwa kutatizwa na ukungu huku helikopta ikiendelea kuwarejesha watu kwenye maeneo usalama