Abdalla Mohamed ajiondoa kusailiwa wadhifa wa kamishna wa IEBC

Mmoja wa waliotuma maombi ya kusailiwa kuhudumu kuwa makamishna wa tume ya uchaguzi ya IEBC nchini, amejiondoa kwenye mchakato huo kuhusiana na stakabadhi bandia za masomo.

Akitangaza hayo Jumatano asubuhi kabla ya shughuli ya kuwasaili waliotuma maombi ya kuhudumu kwenye nyadhifa nne za makamishna wa tume hiyo zilizo wazi kuanza, mwenyekiti wa jopo la kuwasaili Dkt. Elizabeth Muli alisema jopo hilo liliwasiliana na vyuo vikuu na taasisi nyingine kubaini uhalali wa shahada za waliotuma maombi ya kuhudumu kwenye nyadhifa hizo na chuo kikuu cha Methodist kikabaini kuwa Abdalla Mohamed hakupata shahada kutoka taasisi hiyo kama ilivyodaiwa.

Also Read
Vihiga Queens wanyakua kombe la Cecafa baada ya kuwalemea CBE 2-1 na kufuzu kwa ligi ya mabingwa Afrika nchini Misri
Also Read
IEBC yakamilisha maandalizi ya chaguzi ndogo mbali mbali nchini

Mohamed alikuwa amepangiwa kusailiwa leo kuanzia saa tatu unusu asubuhi.

Dr. Abdirizak-Arale-Nunow akihojiwa katika wadhifa wa kamishna wa tume ya IEBC.

Muli alisema walimfahamisha Abdalla kuhusu majibu hayo ya chuo kikuu cha Methodist tarehe 6 mwezi huu.

Also Read
Mpiga kura aelekea Mahakamani kusimamisha uchaguzi mdogo wa Ugavana Nairobi

Jopo hilo kinatarajiwa kumsaili Dr. Abdirizak Arale Nunow,aliyekuwa wa pili kuorodheshwa kusailiwa akifuatiwa na Anne Mwikali Kiusya mwendo wa saa nane alasiri.

Watu 36 walioorodheshwa kuhojiwa ili kujaza nafasi za makamishna watatu katika tume ya IEBC.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi