Abel Kipsang na Noah kibet watamba Doha Diamond League

Bingwa wa dunia katika mita 1500 katika mashindano ya ukumbini Abel Kipsang na mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 800 katika mashindano ya dunia ya ukumbini ,Noah Kibet ndio Wakenya wawili pekee waliotwaa ushindi kwenye mkondo wa kwanza wa mashindano ya Diamond League mjini Doha Qatar Ijumaa usiku.

Kipsang alishinda mbio za mita 1500,wiki moja tu tangu atawazwe bingwa katika mashindano ya Kip Keino Classic akistahimili ukinzani mkali kutoka kwa bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot aliyemaliza wa pili.

Kipsang alikata utepe kwa dakika 3 sekunde 35 nukta 70 akifuatwa na Cheruiyot kwa dakika 3 sekunde 36 nukta 16 huku Tedesse Lemmi kutoka Ethiopia akiambulia nafasi ya tatu kwa dakiak 3 sekunde 37 nukta 6.

Also Read
Serikali kuwahesabu watu wanaoishi na ulemavu nchini

Noah Kibet ambaye anazidi kuimarika kila kuchao alishinda mbio za mita 800,akiziparakasa kwa dakika 1 sekunde 49 nukta 8 ,ukiwa ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya Diamond league .

“Naskia vizuri ,sikutarajia kushinda .Namshukuru meneja wangu kwa kunipa fursa hii.Nafurahia kuwaona Wakenya wengi huku wakiniunga mkono na naangazia mashindano ya dunia”akasema Kibet

Peter Bol wa Australia alichukua nafasi ya pili kwa dakika 1 sekunde 49 nukta 35 huku Marco Arop wa Canada akiridhia nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 1 sekunde 49 nukta 51.

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji Soufiane El Bakkali aliendelea kudhihirisha ubabe wake aliposhinda utepeni akitumia dakika 8 sekunde 9 nukta 66,akifuatwa na Lamecha Girma wa Ethioipia kwa dakika 8 sekunde 9 nukta 67 huku Abraham Kibiwott akimaliza wa tatu akitumia muda wa dakika 8 sekunde 16 nukta 40.

Also Read
Curtis Olago kuifunza Chipu kwa miaka miwili

Mshindi wa mwaka jana wa diamond league Francine Niyonsaba kutoka Burundi alijikaza kisabuni na kushinda mbio za mita 3000 ,akimbwaga bingwa wa Olimpiki wa mita 1500 Faith Kipyegon katika mzunguko wa mwisho akivuka mstari wa mwisho kwa dakika 8 37 nukta 71.

Kypyegon alichukua nafasi ya pili kwa dakika 8 sekunde 38 nukta 5 wakati Jessica Hull wa ustralia akikamilisha tatu bora kwa dakika 8 sekunde 40 nukta 97.

Also Read
Wakenya wachache kushiriki mkondo wa pili wa Birmingham Diamond League Jumamosi

Katika mbio za mita 200 wanaume Noah Lyles alinyakua ushindi akifyatuka kwa sekunde 19 nukta 72 ,akifuatwa na Fred Kerley wa Marekani kwa sekunde 19 nukta 75 naye Jereem Richards wa Trinidad na Tobago akachukua nafasi ya tatu kwa sekunde 20 nukta 15.

Mbio za mita 200 kwa vipusa zilishindwa na Gabrielle Thomas wa USA aliyetimka kwa sekunde 21 nukta 98 akifuatwa na Shericka Jackson wa Jamaica kwa sekunde 22 nukta 7,wakati bingwa wa dunia Dina Asher Smith wa Uingereza akiambulia nafasi ya tatu kwa sekunde 22 nukta 37.

Mkondo wa pili wa Diamond League utaandaliwa Mei 21 mjini Birmingham Uingereza.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi