AC Milan walinyakua taji ya ligi kuu nchini Italia-Serie A kwa mara ya 19 Jumapili usiku na la kwanza, baada ya subira ya miaka 11 .
Olivier Giroud alipachika mabao mawili huku Franck Kessie akipachika moja na kuwasaidia Milan kuichabanga Sassuolo ugenini mabao 3 kwa nunge katika mechi ya kufunga msimu na kuzoa jumla ya pointi 86.
Pia ilikuwa sdafa kubwa kwa mshambulizi Zlatan Ibrahovic ambaye alikuwa katika kikosi wakati wa mwisho timu hiyo ikishinda kombe la ligi kuu kwa mara ya 10,na alishinda kombe la pili akiwa na umri wa miaka 40 Jumapili.
Intermilan licha ya kusajili ushindi wa mabao 3 kwa nunge nyumbani dhidi ya Sampdoria walimaliza katika nafasi ya pili kwa pointi 84,nayo Napoli ikachukua nafasi ya tatu kwa alama 79.
Timu za Cagliari ,Geneoa na Venezzia zilishushwa ngazi ,wakati timu mbili za Lecce na Cremonense zikipandishwa ngazi kutoka serie B .