Achebi ahifadhi taji ya WBC uzani wa welter katika mchezo wa Muay Thai

Martin Achebi wa Kenya alihifadhi mkanda wa WBC Muay Thai Africa katika uzani wa welter,  baada ya kumshinda Matias Brayan wa Cape Verde pointi 2-1 kupitia kwa uamuzi wa majaji kwenye mashindano ya Ultra fight, yaliyoandaliwa Jumamosi usiku, katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

Achebi akijivunia uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa nyumbani waliofurika ukumbi wa Bomas,alianza vyema pigano hilo la raundi tano ,akitawala raundi ya kwanza ,lakini akalemewa na mpinzani wake , katika raundi za pili na tatu mtawalia .

Also Read
Shirikisho la soka la wasioskia lapigwa jeki na SportPesa
Achebi akipigana na Matias

Mkenya huyo alirejea ulingoni katika raundi ya nne kwa hamasa kuu na kuhakikisha ameshinda raundi hiyo na ile ya mwisho na kuandikisha historia kuwa bondia wa kwanza wa humu nchini kuhifaddhi
taji ya WBC uzani wa kilo 67.

Hata hivyo mambo yalikuwa magumu kwa Mkenya mwingine Javan Buyu aliyeshindwa pointi 1-2 kwenye pigano la kuwania mkanda wa WBC uzani wa kilo 57 feather na Salim Mbaye kutoka Senegal.

Also Read
Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Buyu alishinda raundi za nne na tano katika pigano lake ,alilolemewa katika raundi tatu za kwanza na mpinzani huyo wa Senegal.

Kwenya mapigano mengine 6 yasiyokuwa ya kuwania mataji, Ben Bottleberg wa Kenya alimshinda mwenzake Brian Kimani katika raundi ya kwanza kupitia knock out katika uzani wa kilo 105.

Jared Oscar wa Kenya alimchapa Bruce Mugerwa wa Uganda katika raundi ya tatu kupitia knock out katika uzani wa kilo 52 ,huku pia Brian Nyambare wa humu nchini akimlemea Mohammed Al Munir kutoka Sudan kwenye raundi ya nne kupitia knock out, naye  Mohammed Ali kutoka Sudan akapata ushindi kwa wingi wa alama dhidi ya Faruk Ogwak wa Uganda .

Also Read
Murkomen, Duale na Wahome wajiuzulu bungeni kuchukua majukumu ya Uwaziri
Javan Buyu akipigana na Salim Mbaye kutoka Senegal

Josiah Lumunya wa Uganda alimshinda Hamza Bounabri kutoka Morocco katika raundi ya pili kwa njia ya Knock out.

Mabondia kutoka Ufaransa ,Uganda,Cape Verde,Senegal ,Morocco,Algeria ,Sudan na wenyeji Kenya walishiriki mashindano hayo yaliyoandaliwa na shirikisho la Muay Thau Africa.

  

Latest posts

Atlas Lions ya Moroko yaiparuza Ubelgiji Kombe la Dunia

Dismas Otuke

Rais Ruto: Kenya ina uwezo wa kujiendeleza kiuchumi

Tom Mathinji

Visa 36 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi