Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Mwanamuziki huyo mzaliwa wa Pwani alikuwa mgeni kwenye kipindi cha runinga ya KBC na Pwani Fm cha Mashav Mashav Leo ambapo watangazaji Ken 1Gb na Makuu walitaka kufahamu ni kwa nini alisalia kimya mwa muda.

Adasa alisema kwamba mvutano kati ya wazazi wake na jamaa zake wengine ndio ulisababisha asalie kimya. Kulingana naye babake mzazi hapendi kwamba amechagua kuwa mwanamuziki angependa azingatie masomo na mamake anamshabikia ila anasubiri siku moja aingilie muziki wa injili.

Also Read
Gladys Erude kuzikwa tarehe 14 Agosti kaunti ya Nandi

Kama zawadi kwa mamake mzazi, Adasa alisema amemwimbia mamake wimbo wa kumsifu na mwingine wa injili.

Hata hivyo Adasa na wazazi wake waliafikia makubaliano kwamba atasoma huku akiendeleza muziki.

Kuhusu kibao chake cha hivi punde kiitwacho “Nisepe”, Adasa anasema kwamba ni hadithi ya tukio halisi maishani mwake. Anasema alidanganyika na usemi wa marafiki kwamba kupendwa ni raha akaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini akaishia kuvunjwa moyo na mpenzi wake. Anasema alimpata akiwa na mwingine ndio akaamua kujitoa.

Also Read
KBC Channel One kuonyesha mechi ya Kenya dhidi ya Comoros Jumatano

Makuu hata hivyo alikuwa na maswali kuhusu ubunifu kwenye video ya kibao hicho ambapo alisema Adasa hakuonekana kama mtu anateseka kwenye mapenzi. Adasa alijitetea akisema alitaka kuhimiza wanaopitia magumu kwenye mahusiano wasijiachilie. Wajipende na kujing’arisha.

Also Read
"Wife Material itakuwa kubwa na bora zaidi" asema Eric Omondi

Adasa alikana tetesi kwamba yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na meneja wake ambaye anaitwa Josky Madala. Anasema hata kama ingekuwa ukweli hakuna ambaye angejua Kwani yeye anapenda kuweka mambo yake Siri.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi