AFC Leopards kumzindua kocha mpya kutoka Ulaya

Mabingwa mara 13 wa ligi kuu Kpl Afc Leopards wanatarajiwa kumzindua mkufunzi mpya Tomas Trucha kutoka Jamhuri ya Czech huku Athony Kimani ambaye amekwua akishikilia wadhfa huo kwa muda akishushwa madraka.

Kulingana na fununu kutoka ngome ya Ingwe  Trucha atasaini kandarasi ya miaka miwili huku Kimani akiwa msaidizi wake .

Also Read
Mashabiki 10,000 kuingia Nyayo kwa mechi ya Gor Mahia dhidi ya Otoho Jumapili

Trucha aliye na miaka 49 amekuwa mazoezini na Leopards kaunzia mapema wiki hii huko Iten Kaunti ya Elgeyo Marakwet tangu awasili nchini wiki jana na atamrithi Andre Casa Mbung’o wa Rwanda aliyejiuzulu Desemba mwaka jana kwa kutolipwa mshahara wake.

Also Read
Ulinzi Stars yaifyatua Leopards na kuchupa kileleni pa ligi kuu ya Kenya

Mkufunzi huyo amekuwa akiinoa timu ya Township Rollers ya Botswana kabla ya kutua  Leopards na atakuwa na jukumu la kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu mpya utakapoanza mwezi ujao ,wakiwinda kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998.

Also Read
Leopards wanoa kucha kwa kumsajili chipukizi Bienvenue

Leopards walio katika mazoezi ya nyanda za juu mjini Iten pia wanatarajia kuwazindua wachezaji wao wapya Jumatatu ijayo.

  

Latest posts

Msimu mpya wa ligi kuu ya FKF waahirishwa kutoka Oktoba Mosi

Dismas Otuke

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

FIVB:Kenya yatimuliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha Italia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi