AFCON kuandaliwa baina ya Januari 9 na Februari 6 mwaka ujao nchini Cameroon

Makala ya 33 ya mashindano ya kuwania kombe la mnataifa ya Africa AFCON yataandaliwa nchini Cameroon baina ya Januari 9 na Februari 6 mwaka ujao.

Kulingana na kikao cha baraza kuu la CAF kupitia kwa njia ya mtandao droo ya kipute hicho itaandaliwa juni 25 mwaka huu , ambapo timu 24 zitagawanywa kwa makundi 6 ya timu nne kila moja .

Also Read
FKF yakosolewa kwa kumtimua kocha Jacob Mulee wakati usiofaa

Mataifa 23 yamejikatia tiketi kwa kindumbwendumbwe hicho cha mwakani ,huku nafasi moja iliyosalia ikijazwa na aidha Sierra Leone au Benin zitakapochuana mwezi kati ya Mei 31 na Juni 5 mwaka huu ,baada ya pambano hilo kuahirishwa wiki jana baada ya wageni Benin kuteta kuhusu matokeo ya Covid 19 kwa wachezaji wake.

Also Read
Kenya Comoros vikosi vyatajwa

Timu zilizowahi tiketi ya mashindano ya mwakani nipamoja na mabingwa watetezi Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Comoros, Egypt, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Ivory Coast, Malawi, Mali, Mauritania, Morocco, Nigeria, Senegal, Sudan, Tunisia na Zimbabwe .

  

Latest posts

Tusker kushikana mashati na Gor Mahia mechi ya kufungua pazia la msimu kuwania kombe la supa

Dismas Otuke

Isabella Mwampambo mkuzaji vipaji vya soka Upendo Friends Sports Academy mjini Arusha Tanzania

Dismas Otuke

Shujaa yashindwa fainali ya kombe kuu na Afrika Kusini 5-38 Vancouver 7’s

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi