Afisa wa KDF atiwa nguvuni kwa kumnajisi mtoto wa miaka 12

Afisa mmoja wa vikosi vya ulinzi KDF, ametiwa nguvuni baada ya kumnajisi msichana wa umri wa miaka 12 katika eneo la Langas kaunti ya Uasin Gishu.

Kulingana na maafisa wa uchunguzi wa Jinai DCI, ” Afisa huyo Private, Elly Kipkoech,wa kitengo cha 9KA, Second Brigade, kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Langas, kwa kumnajisi msichana wa umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba mjini Eldoret,”.

Also Read
Washukiwa wawili wa ujambazi wauawa na Polisi kaunti ya Kiambu

Msichana huyo aliyefika nyumbani Jumamosi saa moja na nusu usiku, alimwambia mamake mzazi kuwa alichelewa baada ya kutekwa na mwanaume mmoja aliyemdhulumu kimapenzi.

Also Read
Mwanamke tapeli akamatwa Mombasa kwa wizi wa shilingi milioni 1.7

Baada ya uchunguzi zaidi, mamake aligundua damu katika nguo za ndani za msichana huyo.

Baada ya kuripoti kwa maafisa wa polisi, maafisa wa DCI walimsaka na kumfumania mshukiwa katika mtaa wa Green Park alikokwenda mafichoni  na kumtia nguvuni.

Private Elly Kipkoech kwa sasa anatayatishwa kufunguliwa mashtaka Kulingana na sheria za kijeshi baada ya kutambuliwa na mwathiriwa.

Also Read
Wawaniaji nyadhifa za kisiasa kuwasilisha majina ya vyama vyao kabla tarehe 26 Mwezi Machi

Wawili hao wamefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika hospitali ya rufaa na matibabu ya Moi.

”Idara ya DCI Iko katika tahadhari kuu kufuatia ongezeko la dhuluma za kimapenzi na imejitolea kuwatia nguvuni wahusika wote bila kujali nafasi zao katika jamii,” ilisema DCI.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi