Afrika Kusini yatangaza kanuni mpya za kukabiliana na COVID-19

Afrika Kusini imetangaza kanuni mpya za kudhibiti wimbi la pili la msambao wa ugonjwa wa COVID-19.

Rais Cyril Ramaphosa amesema kiwango cha juu cha maambukizi mapya ya ugonjwa huo kimezua hofu kubwa kwa hivyo akatangaza kanuni za kufunga fuo na kudhibiti mikusanyiko ya watu msimu wa sherehe.

Vijana nchini humo wamelaumiwa kwa kuchochea wimbi jipya la maambukizi ya COVID-19 kutokana na tabia zao za kukusanyika kwenye karamu na tafrija za kunywa mivinyo.

Also Read
Watu 1,130 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Rais Ramaphosa amesema takriban vijana elfu moja walithibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona siku moja pekee baada ya karamu hiyo ya ufuoni.

Also Read
Maseneta wa Marekani wapitisha mswada wa dola trilioni 1.9 za kukabiliana na athari za korona

Amesema fuo katika majimbo kadhaa, isipokuwa zilizoko karibu na Jiji la Cape Town, zitafungwa msimu huu wa sherehe.

Muda wa amri ya kutotoka nje pia utaongezwa kuanzia saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri.

Idadi ya watu watakaoruhusiwa kuhudhuria mikutano ya kijamii itapunguzwa hadi watu mia moja kwa kila sherehe za nyumbani na watu 250 kwa kila sherehe za nje, huku mikutano ya kupanga mazishi ikipigwa marufuku.

Also Read
Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Ramaphosa ameonya kuwa wimbi la pili la COVID-19 huenda likawa kali kuliko lile la kwanza iwapo watu hawatazingatia kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa huo.

  

Latest posts

Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Tom Mathinji

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai nchini Tanzania afungwa miaka 30 gerezani

Tom Mathinji

Mbunge Sir David Amess auawa kwa kudungwa kisu nchini Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi