Afueni baada ya tume ya kudhibiti kawi kupunguza bei za mafuta nchini

Halmashauri ya kudhibiti kawi na mafuta (EPRA) imetangaza kupungua kwa bei za lita moja ya mafuta ya petrol ya super, diseli na mafuta taa.

Bei ya lita moja ya petroli  ya super imepungua kwa shilingi  1.42.

Katika jiji la Nairobi lita moja ya petroli ya super inauzwa kwa bei ya reja reja ya shilingi  105.85 na shilingi  103.45 mjini Mombasa.

Also Read
Tume ya EPRA yaongeza bei za mafuta humu nchini

Lita moja ya petroli ya super Nakuru itagharimu shilingi  105.56. Bei ya juu zaidi ya lita moja ya mafuta itakuwa katika kaunti ya Mandera ambapo lita moja itauzwa kwa shilingi 118.89.

Bei ya lita moja ya mafuta ya diseli imeshuka kwa shilingi 2.21 Jijini Nairobi ambapo sasa itauzwa kwa shilingi  90.70 huku ikiuzwa kwa shilingi 88.31 mjini  Mombasa na shilingi 90.63 mjini Nakuru .

Also Read
Bei ya mafuta yaongezwa hapa nchini

Mafuta hayo yatauzwa kwa bei ya juu zaidi katika eneo la Mandera ambapo yatauzwa kwa shilingi 103.73.

Also Read
Mashahidi 37 kushuhudia dhidi ya Okoth Obado katika kesi ya mauaji ya Sharon Otieno

Bei ya mafuta taa pia imeshuka kwa shilingi 2.10 na sasa lita moja ya mafuta taa jijini Nairobi itauzwa kwa shilingi 81.63, shilingi 79.25 mjini Mombasa na shilingi  82.51 mjini Eldoret.  

Bei ya juu zaidi ya mafuta hayo itashuhudiwa katika eneo la Mandera ambapo itauzwa kwa shilingi  94.67 .

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi