Agnes Tirop aweka rekodi mpya ya dunia ya kilomita 10 ya dakika 30 na sekunde 1 katika

Mkenya Agnes Jebet Tirop  ameweka rekodi mpya dunia ya  wanawake pekee ya dakika 30 na sekunde 1 , katika  mbio za kilomita 10   za  adizero road  to road records  mapema Jumapili mjini  Herzogenaurach nchini Ujerumani.

Tirop ambaye pia  ni bingwa wa dunia wa mbio za nyika  mwaka 2015 , ameboresha rekodi ya awali ya dunia kwa sekunde 28  alipotimka na kuwacha wapinzani  wake akiwemo Sheila Chepkurui  katika kilomita mbili za mwisho.

Also Read
Prague kuandaa shindano jipya la Marathon kwa timu Mei 30

Tirop amevunja rekodi yake TiAsmae Leghzaoui wa Moroko ya dakika 30 na skeunde 29 iliyoandikishwa mwaka 2002.

Chepkurui amemaliza katika nafasi ya pili kwa dakika 30 na sekunde 17  huku  nancy Jelagat akitwaa nafasi ya tatu kwa dakika 30 na sekunde 50.

Also Read
Kipsang' asajili rekodi mpya ya Olimpiki na kuingia fainali ya mita 1500 sawia na Cheruiyot wakati Simotwo akifungiwa nje
Agnes Tirop wakiwa na Sheila Chepkurui baada ya mbio

Mbio za wanaume zimeshindwa na Mkenya  Rhonex Kipruto aliyetumia dakika  26 na sekunde 43, ambao ni muda wa nne wa kasi kwenye historia  , akifuatwa na bingwa wa dunia kwa chipukizi wasiozi umri wa miaka 20 Tadese Worku wa Ethiopia kwa dakika  26 na 56  huku Kennedy Kimutai kutoka kenya akimaliza wa tatu kwa dakika 27 na  9..

Also Read
Magari ya uchukuzi wa umma yaanza kubeba Idadi ya kawaida ya abiria

Abel Kipchumba  pia wa Kenya ameshinda mbio za  nusu marathon kwa kuziparakasa kwa dakika  58 na sekunde 48 akifuatwa na  Alexander Mutiso Munyao kwa dakika  59 na sekunde 20.

Brenda Jepleting ameendeleza ubabe wa Wakenya aliposhinda mbio za nusu marathon kwa akina dada akisajili saa 1 dakika 6 na sekunde 52 .

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi