Ain’t no Peace, Kibao kipya cha Akon

Mwanamuziki wa Marekani kwa jina Akon alizindua Kibao kipya kwa jina “Ain’t no Peace” au ukipenda” hakuna amani”.

Katika wimbo huo Akon anazungumzia ukosefu wa amani katika barabara za Marekani pale watu weusi wanapo dhulumiwa na polisi. Aliaune Damala Badara Akon Thiam ni mmarekani mwenye asili ya nchi ya Senegal.

Akiwa anapeperusha bendera ya Amerika Akon anawahimiza wamarekani weusi kukataa kudhulumiwa.

Also Read
Medali ya Uhuru - Dolly Parton

Kinachosisimua zaidi ni maigizo kwenye video ya Kibao hicho.

Mwanamuziki Akon analeta picha inayozua swali la ‘ingekuwaje Kama watu weusi ndio wangekuwa wanadhulumu wazungu?’

 

Video inaanza na Akon mwenyewe akiwa amesimamishwa na Askari mzungu ambaye anatishia kumpiga risasi wanang’ang’ania bastola na risasi inafyatuka Ila haijulikani ilimpata Nani.

Kati Kati kuna mabwanyenye wa asili ya Afrika ambao wanakagua vijakazi wazungu.

Also Read
Mamito apeleka ucheshi nchini Tanzania

Sehemu nyingine pia kuna Mama mkongwe wa asili ya Afrika ambaye anaona mtoto mzungu nje ya makazi yake anamwitia polisi ambaye anampiga tu risasi bila hata kufikiria.

Akon anahimiza raia wa Marekani na sehemu zote ulimwenguni wabadili mawazo. Wachukulie watu weusi Kama binadamu na waache kuwadhulumu.

Mwanamuziki Akon ambaye anamiliki kampuni ya muziki kwa jina “Konvict Muzik” ambayo ilisimamia wasanii maarufu kama Lady Gaga na T pain wakati fulani.

Also Read
Ashanti azuru Kenya

Mnamo mwezi mei mwaka huu, polisi nchini Amerika walishtumiwa kwa kifo cha Bwana George Floyd jambo ambalo lilisababisha maandamano kote nchini Amerika na sehemu zingine ulimwenguni.

Kauli mbiu ilikuwa “Black lives matter” kwa nia ya kusisitiza thamani ya maisha ya watu weusi.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi