Ajali ya treni yasabaisha lita 750,000 za mafuta ya mawese kumwagika mto Kambu

Halmashauri ya maji imewatahadharisha watu wanaoishi kando-kando ya mto Kambu,Kaunti ya Makueni wasiyatumie maji ya mto huo baada ya treni kumwaga lita alfu 750 za mafuta ya mawese kwenye eneo hilo.

Maji ya mto huo ambayo huelekea mtoni Athi hutegemewa mno na wakazi wa eneo hilo kwa matumizi ya nyumbani na unyunyiziaji maji mashambani.

Also Read
Gavana Kibwana azindua mradi wa sola wa shilingi milioni 58

Halmashauri hiyo imetoa ilani hiyo kwa wakazi katika sehemu maalum na katika vituo vya kibiashara, siku mbili baada ya ajali hiyo ya treni katika reli ya zamani.

Also Read
Madaktari waibua wasi wasi kuhusu kufurika kwa wodi za wagonjwa mahututi

Mwenyekiti wa kamati ya mazingira katika bunge la Kaunti ya Makueni, Joseph Muema na afisa mkuu anayesimamia mazingira Mary Mbenge, walionya kuwa mafuta hayo yana madhara mengi kwa mazingira.

Also Read
Kenya yaripoti visa vipya 130 vya COVID-19, wagonjwa 106 wapona na 5 waaga

Maafisa hao wametoa wito kwa shirika la reli humu nchini kulinda sehemu yalikomwagika mafuta hayo huku wakionya wakazi dhidi ya kuyatumia mafuta hayo.

  

Latest posts

Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,335 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Nyumba za thamani ya shilingi milioni 10 zabomolewa Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi