Akon azuru Uganda

Mwanamuziki na mfanyibiashara wa Marekani mwenye asili ya Senegal Aliaune Damala Badara Akon Thiam maarufu kama Akon jana alitua nchini Uganda kwa kile alichokitaja kuwa ziara ya kibiashara.

Alitangaza ziara hiyo yake kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alipachika picha zinazomwonyesha yeye na mke wake wakiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mke wake Janet katika ikulu ya Rwakitura.

Also Read
Akon aingilia biashara ya madini nchini Congo

Kwenye maelezo ya picha hizo, Akon alisema kwamba walikwenda kutafuta fursa za biashara katika taifa hilo la Afrika mashariki na analenga sekta za nishati, utalii na maendeleo ya miundombinu.

Akiwa humo alipata kukutana na watu wengine akiwemo mwanamuziki Eddy Kenzo na akaswali pia kwenye msikiti wa kitaifa wa Gaddafiambapo alikutana na kiongozi wa dini Sheikh Shaban Ramadhan Mubaje.

Also Read
Meghan Markle aandika kitabu cha watoto

Chini ya picha zake na Eddy Kenzo mtumiaji mmoja wa Facebook kwa jina “Jothan Ug” alimwomba Akon azungumze na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusu wanamuziki waliotiwa mbaroni wakati wa uchaguzi kama vile Nubian Li na Dan Magic.

Also Read
Kukamatwa kwa 'Bobi Wine' nchini Uganda kwa sababisha maafa ya watu watatu

Alimwomba asihi Rais awaachilie huru pamoja na wafuasi wengine wa mwanamuziki na mwanasiasa Bobby Wine.

Akon alianza na biashara ya muziki na baadaye akaingilia biashara nyingine kama vile ya madini ambapo anamiliki mgodi wa Almasi nchini Afrika Kusini.

Na nyumbani nchini Senegal, anajenga jiji kwa jina Akon ambalo anasema litagharimu dola bilioni sita za Marekani.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi