Akothee Alalamika Kuhusu Tabia za Mashabiki

Mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth Kokeyo maarufu kama Akothee amelalamika kuhusu hulka za mashabiki wake anapokuwa katika sehemu za watu wengi. Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii mwanamuziki huyo amesema kwamba anajuta kwa kuwa mtu maarufu. Haya yanajiri baada ya kile alichokitaja kuwa kuviziwa na mashabiki ambao badala ya kumsalimia wakimwona huchagua kumrekodi kwa simu zao za rununu.

Also Read
"Napenda miguu yangu" Lupita Nyong'o

Anasema wakati fulani akiwa kwenye duka la jumla na familia yake, karibu apigane na mmoja ambaye alikuwa amerekodi video ndefu ambayo anafananisha na filamu. Kulingana na Akothee, shemeji yake ndiye aliona shabiki huyo akirekodi video na alipomuuliza akawa mjeuri akalazimika kuingilia.

Also Read
Tanasha Donna kuzindua Albamu yake mwakani

Akothee amegusia pia mashabiki ambao wanataka kupiga naye picha wakati huu ambapo anaugua na analazimika kutumia kifaa cha kunyoosha shingo na uso wake umefura akisema wanafaa kusubiri hadi apone. Mwisho wa mwaka jana mwanamuziki huyo alililazwa hospitalini mara kwa mara lakini hakutangaza alochokuwa akiugua.

Also Read
Vanessa Bryant aungwa mkono na watu wengi maarufu

Haya yanajiri wakati ambapo mwanamuziki huyo anaomboleza kifo cha mmoja wa wafanyikazi wake kwa jina “Charo” ambaye anasema alikwenda kulala na hakuamka. Mzazi huyo wa watoto watano anashindwa kilichosababisha kifo cha Charo akishangaa atakayetunza mke wake na watoto na pia kuendeleza kazi yake.

  

Latest posts

Rais Samia Alivyosherehekewa Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Marion Bosire

Azimio la Bien Barasa Mwaka Huu

Marion Bosire

Anne Kansiime Afiwa na Baba Mzazi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi