Akothee amsifia YY

Mwanamuziki na mjasiriamali wa Kenya Esther Akoth maarufu kama Akothee amemsifia mchekeshaji Oliver Otieno maarufu kama YY.

Hii ni baada ya mchekeshaji huyo kuchapisha picha ya nyumba ambayo amemjengea mamake mzazi huku akifananisha na aliyokuwa akiishi awali. Chini ya picha hizo YY aliandika “Nakupenda Mama yangu”.

Akothee alichukua picha hizo akazipachika kwenye akaunti yake ya Instagram akisema Yy amefanya kitu ambacho wengi hawajafanya. Kulingana naye wapo wananaume ambao wanaendesha magari ya kifahari mjini wasijue wanakolala wazazi wao.

Alimtania mchekeshaji huyo akimuuliza umri wake na ni kwa nini hakuchagua kutumia pesa hizo kwenda likizo hata kama ni Dubai.

Alimsifia akisema “Umecheza kama wewe, na vile industry ni ngumu”.

Yy na wachekeshaji wengine bila kusahau wanamuziki hutegemea kutumbuiza kwenye mikusanyiko ndipo wapate riziki lakini tangu ujio wa janga la Corona, wasanii hawajapata nafasi hizo Kwani mikusanyiko imepigwa marufuku.

Ubunifu sasa ndio njia ya pekee ambapo wengi wamegeukia kuunda video na kuzisambaza kupitia majukwaa ya mitandaoni kama You Tube ili wapate kulipwa. Wengine wameingilia kazi ya kutangaza bidhaa na biashara za watu kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii baada ya kulipwa.

  

Latest posts

Betty Bayo Afichua Sura ya Mpenzi Wake

Marion Bosire

Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Marion Bosire

Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi