Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Mwanamuziki Esther Akoth maarufu kama Akothee ametangaza kwamba mke wa waziri mkuu wa zamani Bi. Ida Odinga amekubali kuwa mgeni wa heshima kwenye hafla ambayo anapanga.

Akothee ambaye anaonekana kupumzika kwa muda kutoka kwa muziki anaandaa sherehe ya mwaka mmoja wa kuwepo kwa wakfu wake uitwao “Akothee Foundation”. Mama huyo wa watoto watano alipachika picha akiwa na Mama Ida na kumshukuru kwa kukubali wito wake wa kuongoza hafla hiyo ya tarehe 25 mwezi Septemba mwaka huu wa 2021 katika hoteli ya Kempiski.

Also Read
Siku nitakufa mnizike mara moja! Akothee

Wakfu wa Akothee ulizinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2019 katika hoteli ya Weston Nairobi na angesherehekea mwaka mmoja wa uwepo wake mwaka jana lakini hilo halikufanyika labda kwa sababu ya janga la Corona.

Also Read
Heri hamngekuja! Akothee afokea wageni

Kupitia wakfu huo, Akothee amekuwa akisaidia makundi kadhaa ya wasiobahatika katika jamii. Aliwahi kupeleka misaada ya chakula na matangi ya maji katika eneo la Turkana na huwa pia anafadhili masomo ya wanafunzi wasiojiweza katika jamii.

Usaidizi wake hata hivyo uliwahi kumtongea ambapo mwezi Novemba mwaka jana alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kwamba alikuwa amekatiza usaidizi kwa jamaa mmoja kwa jina Shadrack Mwita ambaye alikuwa amemchukua kama mtoto wake. Mwita ambaye ni mlemavu anasemekana kutoa mahitaji magumu kwa Akothee baada ya Akothee kumpa makazi.

Also Read
Chipukeezy ateuliwa naibu mwenyekiti wa bodi ya NACADA

Mwita anasemekana kugura nyumba ambayo Akothee alikuwa amempangishia akitaka Akothee akajengee nyanyake nyumba kati ya mahitaji mengine mengi.

  

Latest posts

Arrow Bwoy Amefiwa

Marion Bosire

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi