Akuapem Poloo aachiliwa kwa dhamana

Mahakama moja mjini Accra nchini Ghana ilimwachilia muigizaji Rosemond Alade Brown maarufu kama Akuapem Poloo jana kwa dhamana ya Cedi elfo 80 pesa za Ghana.

Sharti moja la dhamana hiyo ni kwamba anastahili kufika kwa afisi ya mchunguzi wa kesi yake baada ya kila wiki mbili na jingine ni kupeleka pasipoti yake kwa msajili wa mahakama.

Awali mwanadada huyo alikuwa amehukumiwa kifungo cha siku 90 gerezani na mahakama tofauti kwa kosa la kuvujisha picha zake akiwa uchi kwenye mitandao ya kijamii.

Also Read
Chadwick Boseman ashinda tuzo la Golden Globe

Wengi wa wafuasi wa muigizaji huyo walilalamikia adhabu hiyo wakisema ni kali mno huku wengine wakisema ilikuwa sawa kulingana na kosa lake.

Waigizaji wengi walionekana kuomba Akuapem aachiliwe huru ili akatunze mtoto wake kwani ni yeye mlezi wake wa pekee. Tonto dike wa Nollywood Nigeria ni mmoja wa walioomba Akuapem aachiliwe akisema alichokifanya ni kinyume na maadili lakini hakitoshi kumpeleka jela.

Also Read
Onyesho la mitindo ya mavazi laahirishwa Rwanda

Kwa upande mwingine alionekana kumtetea akisema hakuna mtu atakayefunza mama yeyote kuhusu jinsi ya kulea mtoto wake isipokuwa pale mtoto huyo anapoumizwa na mienendo ya mzazi wake.

Tonto wa umri wa miaka 35 alikuwa ameomba watu wa taifa la Nigeria watie saini ombi la mitandaoni la kutafuta kuachiliwa huru kwa Akuapem Poloo ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume sawa na yeye.

Also Read
Meghan Markle aandika kitabu cha watoto

Picha za pamoja za muigizaji huyo akiwa uchi na mtoto wake mvulana zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakihisi kwamba alikuwa amevuka mpaka kwa kupiga picha uchi na mwanawe wa kiume wa umri wa miaka 7.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi