Mchekeshaji Mannerson Uduor Ochieng maarufu kama Akuku Danger amepata Nafuu. Alizungumza akiwa kwenye kitanda cha hospitali kwenye video iliyochapishwa na Sandra Dacha ambaye ni muigizaji.
Akuku aligonjeka mwisho wa mwaka jana ambapo alipelekwa hospitalini akapata nafuu akarejea nyumbani na akagonjeka tena siku chache baadaye ambapo alikimbizwa hospitalini na ikabainika kwamba mapafu yake yalikuwa yanafifia.
Alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji usaidizi wa mashine kupumua lakini sasa amehamishiwa wodi ya kawaida.
Siku ya mkesha wa kukaribisha mwaka 2022, Daniel Ndambuki maarufu kama Churchill alitangaza alichokuwa akiugua Akuku Danger na ni ugonjwa wa seli mundu yaani sickle cell anemia ambao alizaliwa nao.
Kwenye hafla hiyo ya mwaka mpya, Churchill aliwarai mashabiki wake wakatoa mchango wa kugharamia matibabu ya Akuku Danger fedha ambazo zimesaidia pakubwa ila bado kuna deni la bili ya hospitali.
Wasanii hasa wachekeshaji, waigizaji na hata wanamuziki wamekuwa wakiomba mchango kwa niaba ya mwenzao kupitia mitandao ya kijamii.
Akuku Danger anafaa kuruhisiwa kuondoka hospitalini wakati wowote ila kwanza lazima alipe bili yote.
Ili kutoa mchango wako kwa ajili ya gharama ya matibabu ya mchekeshaji Akuku Danger katika hospitali ya Nairobi West fuata maagizo kwenye bango hili;