Albamu mpya ya Kanye West

Albamu ya Kanye West ambayo imesubiriwa kwa hamu inatarajiwa kutoka leo Ijumaa tarehe 23 mwezi Julai mwaka 2021.

Mwanamuziki huyo wa Marekani aliandaa kikao cha kusikiliza nyimbo ambazo ziko kwenye albamu hiyo katika uwanja wa michezo wa Mercedes Benz huko Atlanta.

Watu wapatao elfu 42 walihudhuria kikao hicho na kila mmoja alilipa ada ya kuingia ya Kati ya dola 20 hadi 100, sawa na shilingi elfu 2 hadi elfu kumi za Kenya.

Also Read
Cardi B azawadi mume wake gari la kifahari

Ilivyo kawaida yake, Kanye alichelewa kufika kwenye kikao hicho ambacho kilikuwa kimepangiwa kuanza saa mbili usiku kulingana na saa za Marekani.

Alifika saa nne kasoro dakika kumi na hakuimba wala kusema lolote. Alionekana tu akizunguka zunguka uwanjani huku akiwa amevalia mavazi ya rangi nyekundu.

Also Read
Babu ya Burna Boy ampongeza kwa Grammy

Mpango mzima wa kusikiliza nyimbo za albamu ya Donda ulichukua muda wa dakika 48.

Donda ni jina la marehemu mamake Kanye West ambaye aliaga dunia mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 58.

Waliohudhuria kikao cha kusikiliza albamu wanasema sauti ya marehemu Donda West inasikika ikikatibisha wasikilizaji kwenye wimbo mmoja.

Also Read
Anjella sasa ni mwana Konde Gang

Kanye West awali alikuwa ameahidi kutoa albamu hii mwaka jana mwezi Julai na no hulka ambayo anaonekana kuendeleza, ile ya kukosa kutoa kazi kulingana na muda aliosema.

Haya yanajiri wakati ambapo Kanye West amekubali kumpa talaka Kim Kardashian ambaye ni mzazi mwenzake na amekuwa mke wake.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi