Albamu Mpya ya Kendrick Lamar

Kendrick Lamar mwanamuziki wa mtindo wa rap kutoka nchini Marekani, alitoa albamu mpya hivi maajuzi baada ya subira ya miaka mitano. Kazi hiyo inayofahamika kama “Morales & The Big Steppers” imekuja baada ya ile ya “Damn” ya mwaka 2017 ambayo ilimshindia tuzo ya Pulitzer. Tuzo za pulitzer zilianzishwa mwaka 1917 na huwa zinalenga ubunifu wa hali ya juu katika uandishi wa magazeti, majarida, uandishi wa mitandaoni na utunzi wa nyimbo.

Also Read
LIl Nas X Atoa Wimbo wa Kutusi Waandalizi wa Tuzo za BET

Mr Morales & The Big Steppers inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mitandaoni na alisema ndiyo kazi ya mwisho anafanya chini ya usimamizi wa kampuni ya muziki ya Top Dawg Entertainment. kazi hiyo ina jumla ya nyimbo 18 ambazo amezigawa sehemu mbili, nyimbo tisa tisa. Nyimbo zenyewe ni “United in Grief”, “N95”, “Worldwide Steppers”, “Die Hard”, “Father Time”, “Rich”, “Rich Spirit”, “We cry together” na “Purple Hearts. Sehemu ya pili inajumuisha nyimbo kama vile, “Count me out”, “Crown”, “Silent Hill”, “Savior”, “Auntie Diaries”, “Mr. Morale”, “Mother i sober” na “Mirror”.

Also Read
Siamini Beyonce ni rafiki yangu sasa, Megan Thee Stallion
Also Read
Vaccine, wimbo mpya kutoka kwa Fena Gitu

Kwenye safari yake ya muziki, Kendrick Lamar ambaye ana umri wa miaka 34 sasa ameshinda jumla ya tuzo 161 kutokana na uteuzi mara 399. Tuzo hizo zinajumuisha 14 za Grammy, sita za Billboard Music Awards na ile ya ASCAP Vanguard Award kutokana na utunzi wake.

  

Latest posts

Harusi ya Nandy Kuwa ya Awamu Tatu

Marion Bosire

Mwigizaji Mkongwe wa Nollywood Kenneth Aguba Apata Usaidizi

Marion Bosire

Travis Baker Arejea Kazini

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi