Albamu Ya Mr. Seed

Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya Moses Tarus Omondi maarufu kama Mr. Seed alizindua Albamu yake jana tarehe 12 mwezi Septemba mwaka huu wa 2021 katika hoteli ya Pride Inn eneo la Westlands Kaunti ya Nairobi.

Alifika hotelini humo akiwa kwenye msafara wa magari makubwa ya rangi nyeusi na kisha yeye na mke wake Nimo na mwanao Gold wakashuka wakaelekea kwenye eneo la kupiga picha na kusema na wanahabari.

Also Read
King Kaka Asema Ameugua Kwa Muda

Watatu hao walikuwa wamevalia mavazi ya rangi ya dhahabu ambayo wanasema yaliundwa na Dua Africa Designs. Alipoulizwa ni kwa nini aliamua kumweka mtoto wake Gold Christen Omondi kwenye picha ya Albamu hiyo ambayo inaitwa “The Black Child” Mr. Seed alisema ni kwa sababu yeye ndiye yuko sasa na mwanawe ndiye atakuwa siku za usoni.

Also Read
Studio za Eric Omondi zafungwa

Mwanamuziki huyo alisema kwamba Albamu hiyo ina nyimbo kumi na imeongezwa wimbo mmoja. Kuhusu wanamuziki ambao alihusisha kwenye nyimbo za albamu hiyo, Seed aliamua kuweka siri hadi uzinduzi rasmi.

Mr. Seed ambaye alizaliwa mwaka 1996 ni msanii ambaye amesajiliwa kwenye kampuni ya muziki ya mwanamuziki mwenza Kevin Bahati ambayo inaitwa EMB Records.

Ameafikia ufanisi katika kazi yake kama mwimbaji wa nyimbo za kisasa za injili ingawa safari yake imekuwa pia na misukosuko kadhaa.

Also Read
Weezdom aacha kazi kama meneja wa Bahati

Miezi michache iliyopita, uvumi ulichipuza mitandaoni kwamba alikuwa ameachana na mke wake Nimo ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 8, miaka 6 kama wachumba na miaka 2 kama wanandoa.

Kisa na maana Mr. Seed hakuwa mwaminifu kwenye ndoa na kwamba mwanadada fulani alikuwa na ujauzito wake na sasa amejifungua. Msanii huyo hajasema lolote kuhusu hilo.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi