Albert Wesonga ateuliwa meneja mpya wa AFC Leopards

Msimamizi wa muda mrefu wa soka humu nchini Albert Wesonga ,ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya AFC Leopards ,kuchukua nafasi ya Tom Juma,  ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu meneja tangu Februari mwaka 2020.

Hadi Uteuzi wake , Wesonga amewahihudumu kama meneja wa klabu ya Nakumatt FC,  iliyosambaratika na atakuwa na kibarua kigumu kuinua hadhi ya Ingwe .

Wesonga ameahidi kutumia tajriba yake pana kuleta mwamko mpya klabuni Ingwe ,ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto tele.

Also Read
IEBC yaanza kuwasajili Wakenya wanaoishi ughaibuni kuwa wapiga kura

“Nashukuru kwa uteuzi huu,  na ningependa kuwashukuru  wadau wote wa Leopards,  wakiongozwa na mwenyekiti Dan Shikanda na uongozi mzima wa timu na nitatumia ujuzi na tajriba yangu kuleta matokeo bora .

AFC Leopards ni timu kubwa nchini ambayo ninaihusudu na nimekuwa nikiifuatilia tangu nikiwa mtoto ,kwa hivyo naielewa na tunahitaji kufanya kazi pamoja ili kuleta ufanisi “akasema Wesonga

Also Read
FKF yalalama kuhusu kukosekana kwa viwanja nchini

Ingwe ambao ni mabingwa mara 12 wa ligi kuu nchini KPL ,wanajiandaa kushiriki kwa mashindano ya siku mbili kwa kumbukumbu ya mchezaji wa soka wa zamani wa Ingwe Joe Lidonde,yatakayoshirikisha  vlabu vya Nzoia Sugar FC, Vihiga Bullets na Kakamega Homeboyz yatakayoandaliwa kaunti ya Kakamega.

“Timu yangu ina morali ya juu na tuna imani ya kubeba kombe hili ,huku tukijiandaa kuanza ya mechi za maandalizi kwa msimu mpya “akasisitiza Wesonga

Also Read
Watu wawili zaidi wametolewa katika migodi ya Abimbo

Marehemu Lidonde, aliyefariki Septemba mwaka 1987, alikuwa nahodha wa AFC Leopards na Harambee Stars katika 1950 na 1961.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa shilingi nusu milioni ,timu ya nafasi ya pili shilingi elfu 400 huku ile ya tatu ikienda nyumbani na shilingi elfu 250.

  

Latest posts

Takwimu za kipute 22 cha kombe la dunia nchini Qatar

Dismas Otuke

NPS: Oparesheni ya kiusalama Turkana yazaa matunda

Tom Mathinji

Bodi ya dawa na sumu yapiga marufuku uuzaji wa dawa ya kupanga uzazi ya ‘Sophia’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi