Alice Wahome na Ndindi Nyoro wakaidi maagizo ya polisi

Wabunge wawili kutoka kaunti ya Murang’a  Alice Wahome wa Kandara na  Ndindi Nyoro wa  Kiharu wamesema hawata-tii maagizo ya polisi ya kuwataka kufika katika afisi za idara ya uchunguzi wa maswala ya jinai huko Nyeri kuhusiana na ghasia zilizozuka jumapili mjini Kenol.

Also Read
Naibu Rais William Ruto asema hababaishwi na miungano ya kisiasa inayobuniwa

Wawili hao walijiondoa lawamani na kusema kuwa polisi wanapaswa kuwaita kwanza viongozi waliopanga ghasia hizo ambao walidai kuwa maafisa hao wanawajua vyema.

Wahome na Nyoro walikuwa wametakiwa kufika katika afisi za idara ya upelelezi wa maswala ya jinai huko  Nyeri ili kuwasaidia polisi kwa uchunguzi kufuatia agizo kutoka kwa inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai.

Also Read
COVID-19: Kenya yaripoti visa vipya 366 huku mgonjwa mmoja akiaga dunia

Haya yanajiri huku familia za vijana wawili waliouawa wakati wa ghasia hizo zikitoa wito wa kuharakishwa kwa uchunguzi na kukamatwa kwa wachochezi wa ghasia hizo.

Also Read
Kaunti ya Kiambu kutafiti kuhusu ugonjwa wa Kifafa na madhara yake katika jamii

Christopher Kariuki na  Peter Mbothu walipoteza maisha yao baada ya ghasia kuzuka baina ya makundi mawili hasimu ya kisiasa kabla ya ziara ya naibu wa rais  William Ruto ya kusaidia kuchanga pesa katika kanisa la AIPCA lililoko katika eneo hilo.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi