Aliyekuwa mwanachama wa baraza kuu la shirikisho la soka nchini kutoka eneo la Nyanza , Tom Alila amemtaka waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed kutafuta suluhu ya kudumu kwa tandabelua ,iliyogubika soka ya Kenya,kufuatia hatua ya wiki jana ambapo FIFA iliipiga Kenya marufuku ya muda kwa mwingilio wa serikali katika usimamizi wa kandanda.
Kwenye mahojiano ya kipekee na KBC ,Alila amesema hatua ya FIFA ilitarajiwa lakini pia itasaidia kuleta uongozi bora wa mchezo nchini kufuatia kudorora kwa mchezo huo.
Alila amemwomba waziri Amina kuunda kamati ya muda maarufu kama normalization committee itakayowashirikisha baadhi ya maafisa wa afisi iliyovunjiliwa mbali na wengine wa kamati ya muda kabla ya uchaguzi .
“Ni uamuzi mgumu wa FIFA kuipiga Kenya marufuku ,lakini ulitarajiwa kutokana na hali ilivyokuwa,lakini naiomba FIFA kwa kuwa haipendi ufisadi imruhusu waziri Amina akabiliane na swala hilo na kulitatua kikamilifu ,Waziri atumie hii fursa alainishe kila kitu kwa football yetu”akasema Alila
Alila amefafanua matamshi ya Rais wa FIFA Gianni Infantinho akiipiga Kenya marufu,akisema kile FIFA wanahitaji ni kurejeshwa kwa ofisi kuu ya FKF ,wala sio sharti kurejeshwa kwa Nick Mwendwa.
“Kile FIFA wanataka sio kumrejesha Nick Mwendwa afisini ,lakini ni kurejesha secretariat iliyobaki ofisini baada ya Nick Mwendwa kujiuzulu,sio ati ni lazima Nick arudishwe ofisi”
Sisi kile tunamwomba waziri azungumze na FIFA,na pia kuharakisha care taker commitee iweke mikakati ya uchaguzi then wapeane majina na new office bearers mpira yetu ilirudi normal”akasisitiza Alila
Alila ambaye amejitosa kuwania kiti cha Urais wa FKF ,amesema siri ya kufufua tena sokaa ni kuwekeza katika mipangilio ya soka ya chipukizi,kupitia kwa vituo vya kukuza talanta na kuwekeza zaidi katika mashindano ya shule.