Aliyebadilisha alama ya KCSE kutoka E hadi B- ili apate kazi ya Polisi aishia korokoroni

Polisi wanamzuilia mwanaume mmoja aliyewasilisha cheti chenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyokarabatiwa katika zoezi la usajili wa makurutu.

Jamaa huyo amekamatwa katika eneo la Kihoto, Kaunti Ndogo ya Naivasha baada ya kugundulika kwamba alitumia kalamu kubadilisha matokeo hayo ili atimize matakwa ya kielimu katika usajili huo wa polisi.

Also Read
Moto mkali wateketeza nyumba kadhaa katika mtaa wa Majengo, Nanyuki

Kulingana na taarifa ya polisi, John Mwangi Kimani alipata alama ya E kwenye masomo yote ya mtihani wa KCSE.

Kwa sasa yuko kizuizini akisubiri kufunguliwa mashtaka kwa madai ya kutumia stakabadhi iliyoghushiwa.

Zoezi hilo ambalo limefanyika Jumatatu katika kaunti ndogo zote nchini limelenga kusajili maafisa 5000 wa polisi watakaojiunga na vyuo vya mafunzo mbali mbali humu nchini.

Also Read
Rubani wa kundi la Alshabab asakwa na maafisa wa usalama wa Kenya

Inspekta Jenerali wa Polisi Hilary Mutyambai amesema jumla ya makonstebo 4,700 na makadeti 300 watasajiliwa kwenye zoezi hilo.

Mutyambai alisema kwamba maafisa hao watahudumu katika idara ya polisi kwa kipindi kisichopungua miaka kumi.

Also Read
Wabunge waapa kuunga mkono BBI kwenye warsha ya Naivasha

Aidha, alisema makadeti watakaosajiliwa ni wale waliosomea taaluma za utabibu, uhandisi, masuala ya silaha, elimu na sheria.

Usajili huo unajiri kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao ambapo maafisa zaidi wa polisi wanatarajiwa kupelekwa maeneo mbali mbali kudumisha usalama.

 

  

Latest posts

Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,335 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Nyumba za thamani ya shilingi milioni 10 zabomolewa Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi