Aliyekuwa mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ajitosa katika ulingo wa siasa

Aliyekuwa mtangazaji wa televisheni Mwanaisha Chidzuga, ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge cha Matuga katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Msomaji huyo wa habari wa zamani ambaye ana misururu ya mikahawa jijini Nairobi ni mtoto wa aliyekuwa mwakilishi wanawake wa kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga aliyefariki tarehe 12 mwezi Agosti mwaka 2021.

Akiwahutubia wanahabari nyumbani kwao Golini kaunti ya Kwale, Mwanaisha alisema lengo lake ni kukamilisha ndoto ya marehemu mamake Zeinab Chidzuga aliyetaka kuwania kiti hicho cha ubunge cha Matuga katika uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Gavana wa Nairobi Mike Sonko abanduliwa mamlakani

Wazee na familia wameunga mkono azma ya Mwanaisha huku kakake mkubwa akipinga hatua hiyo.

Kulingana na wazee hao wakiongozwa na Seif Chidzuga, familia hiyo imemwidhinisha Mwanaisha kuridhi uongozi wa kisiasa kutoka kwa marehemu mamake.

Akizungumza katika hafla tofauti, Hassan ambaye ni kakake Mwanaisha alisema dadake anaishi Nairobi na ameolewa Tana River na hivyo hawezi kumrithi mamake kujiunga na siasa.

Also Read
Mhudumu wa bodaboda ahukumiwa miaka 20 gerezani kwa kosa la ubakaji

Mwanaisha alisema azma yake ilichochewa na taaluma yake na kwamba lengo lake kuu ni kusuluhisha matatizo yanayowakumba wananchi.

Mwanaisha aliandamana na viongozi kadhaa wanawake wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa wa maendeleo ya wanawake  Rahab Mwikali.

Mwikali alimsifu marehemu Chidzuga akimtaja kiongozi aliyekuwa na maoni na mjasiri aliyepigania haki za wanawake kwa miaka mingi alipokuwa mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo.

Also Read
Visa 565 zaidi vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

” Tumekuja hapa kuidhinisha ugombeaji wa wa Mwanaisha kwa kuwa tunaamini atajaza pengo lililoachwa na marehemu mamake,” alisema Mwikali.

Mwikali alitoa wito kwa wanawake kukumbatia maswala ya kitaifa kama vile kujitosa katika ulingo wa kisiasa ili kuongeza Idadi yao bungeni.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi