Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, amezikwa Jijini  Algiers bila taratibu zilizozingatiwa wakati wa mazishi ya viongozi waliomtangulia.

Bouteflika ambaye aliondolewa mamlakani mwaka 2019 baada ya maandamano ya umma,  alifariki siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 84.

Also Read
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Algeria na Ufaransa wadorora

Gari la kivita lililopambwa maua lilivuta jeneza lake lililofunikwa Kwa bendera ya taifa hilo kutoka nyumbani kwake Zeralda, magharibi ya mji mkuu wa nchi hiyo, hadi kwenye makaburi ya el-Alia Jijini Algiers ambako watangulizi wake watano wamezikwa.

Familia ya Bouteflika, Rais Abdelmadjid Tebboune na mawaziri wa sasa wa serikali pamoja na maafisa wa jeshi akiwemo mkuu wa majeshi luteni Said Chenegriha, walikuwa miongoni mwa waombolezaji.

Also Read
Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Bouteflika alichaguliwa mara ya kwanza mwaka 1999, na amesifiwa kwa kubuni sera ya kitaifa ya maridhiano iliyorejesha amani nchini humo baada ya mapigano katika miaka ya 90.

Also Read
Guinea yaondolewa katika uanachama wa Muungano wa Afrika

Lakini raia wengi wa Algeria walimlaumu kwa kudorora kwa uchumi katika miaka yake ya baadaye mamlakani wakati hakuwa akionekana hadharani baada ya kuugua kiharusi, na ufisadi ulioenea na kusababisha uporaji mkubwa.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi