Andrew Mwadime ndiye Gavana mpya wa Taita Taveta

Mbunge wa Mwatate, Andrew Mwadime ametangazwa kuwa gavana wa tatu wa kauti ya Taita-Taveta baada ya kujizolea kura 49,901.

Mwadime, ambaye alishiriki kinyang’ayiro hicho kama mgombezi huru, alimshinda gavana wa sasa Granton Samboja, ambaye aliibuka wa pili akiwa na kura 23,703. Mwadime amekuwa mbunge wa Mwatate kwa tiketi ya (ODM) tangu mwaka 2013.

Also Read
Wakulima wa kahawa kaunti ya Murang'a waingilia ukuzaji Macadamia

Kiti cha Ugavana cha eneo la Taita-Taveta, kilikuwa kimevutia wawaniaji 13. Katika hotuba yake ya kuyakubali matokeo, Gavana anayeondoka Granton Samboja alihimiza wakaazi wamuunge mkono Gavana mpya na kumwezesha kusukuma mbele ajenda ya maendeleo.

Also Read
Wapiga kura waliosajiliwa ni milioni 22 nukta 1 yasema IEBC

Kuhusu kinyang’anyiro cha Useneta, Johnes Mwaruma wa chama cha ODM alihifadhi kiti chake baada ya kujizolea kura 39,142.

Mpinzani wakwe wa karibu, Godwin Kilele wa chama cha Jubilee, alipata kura 26,158. Ms. Lydia Haika wa chama cha UDA alihifadhi kiti chake cha mwakilishi wa wanawake baada ya kujizolea kura 38,363.

Also Read
Wanafunzi 38 waambukizwa COVID-19 kaunti ya kitui

Mwakilishi wa zamani wa wanawake Joyce Lay wa chama cha Jubilee alikuwa wa pili baada ya kujinyakulia kura 23,076.

  

Latest posts

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi