Anna Qabale Duba Ashinda Tuzo ya Muuguzi Bora Duniani

Anna Qabale Duba ni mzaliwa wa Kenya hususan kaunti ya Marsabit na anafanya kazi kama muuguzi katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Marsabit. Amegonga vichwa vya habari baada ya kushinda tuzo ya muuguzi bora zaidi ulimwenguni katika hafla iliyoandaliwa huko Dubai. Tuzo hiyo ina pesa pia ambazo ni takriban milioni 27 pesa za Kenya.

Hafla ya kutuzwa iliwiana na siku ya kimataifa ya wauguzi yaani “International Nurses Day” tarehe 12 mwezi Mei siku ambayo imetengwa kutambua mchango mkubwa wa wauguzi katika sekta ya Afya. Anna Duba na mwenzake Jirma Bulle, wote wa asili ya Kenya wanaohudumu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit walijipata kwenye orodha fupi baada ya kusailiwa kwa maombi ya wauguzi wapatao elfu 24 kutoka nchi 180 kwa tuzo hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Aster DM Healthcare ya India.

Also Read
Wafanyibiashara Kajiado wakamatwa na mifuko ya plastiki iliyoharamishwa hapa nchini
Also Read
Zaidi ya magari 100 ya abiria yanaswa kwa kukiuka masharti ya kudhibiti Covid-19 Kiambu

Mwaka 2013, Anna Duba alishinda shindano la ulimbwende linalolenga utalii almaarufu Miss Tourism Kenya. yeye ndiye wa kwanza kufuzu kitaaluma katika kijiji chao na yeye pekee ndiye amefanikiwa kupata elimu kwenye familia yake. Alitumia afisi ya ulimbwende kutekeleza miradi kadhaa ya kusaidia jamii chini ya wakfu wake kwa jina Qabale Duba Foundation. Amesaidia kujenga shule kijijini kwao ambayo inatoa mafunzo kwa watoto asubuhi na jioni kwa watu wazima.

Also Read
Masomo ya darasani yapigwa marufuku hapa nchini

Binti huyo ni mkenya wa pili kushinda tuzo ya kimataifa ya kumezewa mate baada ya Padri mwalimu Peter Tabichi kushinda tuzo ya mwalimu bora zaidi ulimwenguni mwaka 2019. Tabichi hutumia mshahara wake wote kusaidia walio na mahitaji hasa wanafunzi wake. Alituzwa dola milioni moja za kimarekani.

  

Latest posts

Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Tom Mathinji

Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Homa Bay wagoma wakidai kucheleweshwa kwa mishahara

Tom Mathinji

Watu 75 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi