Anne Kansiime amejifungua!

Mchekeshaji wa Uganda Anne Kansiime amejifungua mtoto wa kiume.

Mwanadada huyo alipachika picha akiwa amempakata mtoto wake katika kitanda cha hospitali na kusema kwamba anaitwa “Selassie Ataho”.

Aliongeza kwamba dhambi zake zimesamehewa.

Yapata wiki moja iliyopita, Kansiime alitangazia umma kwamba anatarajia mtoto akisema alikuwa anashindwa jinsi ya kutangaza habari hizo njema.

Also Read
Sammy Kasule aaga dunia

Ijumaa tarehe 16 mwezi huu wa April, Kansiime na mpenzi wake Abraham Tukahiirwa waliandaa tamasha la mitandaoni ambapo alisema ujauzito wake umenyamazisha wakosoaji.

Anne alisema watu wengi walikuwa wakitafuta majibu ya ni kwa nini yeye na mume wake wa awali Ojok hawakuwa wamebarikiwa na watoto kiasi cha kudai kwamba alikuwa ameuza kizazi chake kwa ushirikina.

Also Read
Emmanuella aigiza kwenye filamu ya Australia

Wiki ya mwisho kabla ya kujifungua ilikuwa yenye shughuli nyingi kwa Anne na mpenzi wake, kuanzia kwa kupiga picha za ujauzito, kuunda kitanda cha mwanao hadi kwenye kuandaliwa sherehe ya kukaribisha mtoto na marafiki wake.

Anne Kansiime alikuwa ameolewa na Gerald Ojok Kati ya mwaka 2013 na 2017 walipoachana na hawakuwa na mtoto.

Also Read
Suluhu azuru Uganda kwa mwaliko wa Museveni

Kansiime alifichua kwamba ndoa hiyo haingeendelea kutokana na kukosa watoto na kazi yake ambayo huchukua muda wake mwingi.

Baadaye Anne alitambulisha mpenzi wake Abraham Tukahiirwa maarufu kama Skylanta ambaye ni mwanamuziki lakini wawili hao hawajatangaza ikiwa watafunga ndoa rasmi.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi