Asanteni!

Muigizaji na mchekeshaji wa nchi ya Ghana Rosemond Alade Brown maarufu kama Akuapem Poloo, ameshukuru nyota wawili wa Nigeria ambao walijaribu kumsaidia wakati alikuwa jela.

Aliwataja Mr Eazi ambaye ni mwanamuziki na Mercy Johnson Okojie ambaye ni muigizaji wa Nollywood.

Akuapem alipiga picha mawasiliano ya wawili hao kwenye simu yake na kuzipachika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii akisema aliona mawasiliano hayo baada ya kuachiliwa huru kwani simu zake zilikuwa zimetwaliwa.

Also Read
Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Hata hivyo anawashukuru sana kwa kuonyesha nia ya kumsaidia alipokuwa kwenye kipindi kigumu.

Mwanadada huyo alitiwa mbaroni kwa kile kilichosemekana kuwa ukiukaji wa maadili baada ya kupiga picha akiwa uchi na mtoto wake wa kiume wa umri wa miaka 7 na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Also Read
Emmanuella ajengea mamake nyumba

Baada ya kesi yake kusikilizwa na kuamuliwa, alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu gerezani lakini alikata rufaa na akaachiliwa kwa dhamana.

Kwenye ujumbe wa Whatsapp, Mercy Johnson alikuwa ameandika maneno ya kutaka kujua ikiwa Akuapem yuko salama na ikiwa kuna njia angeweza kumsaidia, huku Mr Eazi akitaka kujua ikiwa alikuwa na wakili na kuonyesha nia ya kumtafutia wakili mwingine.

  

Latest posts

Zuchu Amtania Mamake Khadija Kopa

Marion Bosire

Muigizaji Jaymo Afunga Ndoa

Marion Bosire

Don Jazzy Anatafuta Kumsajili Salle

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi