Asilimia 92 ya vituo vya kupigia kura vimetangaza matokeo ya Urais

Asilimia 92  ya vituo vyote vya kupigia kura nchini  vimetangaza matokeo.

Kulingana na takwimu kwenye  tovuti ya IEBC kufikia Jumatano Alfajiri,jumla ya forms 34A ambazo zinajumuisha matokeo kutoka kila kituo cha kupigia kura yalikuwa yamerekodiwa.

Also Read
Tume Huru Ya Uchaguzi Yasema Iko Tayari kwa Uchaguzi wa Jumanne

Jumla ya vituo vya kupigia kura  42,568  kati ya vituo vote  46,229  ikiwa asilimia 92 kote nchini vimetangaza matokeo kufikia Jumatano saa moja Asubuhi.

Matokeo hayo yatajamuishwa  pamoja katika forms 34B ,ambazo ni jumla ya idadi ya kura zote za Urais kutoka kila eneo bunge kutoka maeneo bunge 290 kote nchini na hatimaye kutolewa kwa forms 34C zinazojumuisha matokeo yote ya Urais katika kila kaunti.

Also Read
Watu wanne wafariki katika ajali ya barabarani Tana River
Also Read
Watu 497 zaidi waambukizwa Corona huku wagonjwa 16 wakiaga dunia

Kulingana na kasi ya juu ya  utoaji wa matokeo ya kura za Urais,huenda tume ya IEBC ikamtangaza mshindi wa kinyang’anyiro  cha ikulu kabla ya muda wa siku saba uliowekwa kisheria.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi